Skip to content Rukia hadi maudhui
nacopha@nacopha.or.tz +255 745 111 242 Dar es Salaam, Tanzania Dar es Salaam, Tanzania

Our work Kazi zetu

Six programme areas, one principle: nothing about people living with HIV without people living with HIV.

Maeneo sita ya programu, kanuni moja: hakuna linaloamuliwa kuhusu watu wanaoishi na VVU bila wao wenyewe.

Advocacy & human rightsUtetezi na haki za binadamu

We take what members experience in clinics, workplaces and communities and turn it into evidence that policy makers cannot ignore - in national HIV strategy, in law reform and in budget hearings.

Tunachukua yale wanachama wanayokutana nayo kliniki, kazini na katika jamii na kuyageuza ushahidi ambao watunga sera hawawezi kuupuuza - katika mkakati wa kitaifa wa VVU, mageuzi ya sheria na vikao vya bajeti.

  • Representation on national HIV coordinating bodiesUwakilishi katika vyombo vya kitaifa vya kuratibu VVU
  • Documenting rights violations reported by membersKuandika ukiukwaji wa haki unaoripotiwa na wanachama
  • Budget tracking for HIV servicesKufuatilia bajeti za huduma za VVU

Treatment literacy & adherenceElimu ya matibabu na kufuata dawa

Starting treatment is not the hard part - staying on it for life is. Trained peer educators walk members through ART, viral load testing and what an undetectable result means.

Kuanza matibabu si sehemu ngumu - kuendelea nayo maisha yote ndiyo changamoto. Waelimishaji rika waliopewa mafunzo huwaelekeza wanachama kuhusu ARV, kipimo cha wingi wa virusi na maana ya kutokuonekana kwa virusi.

  • Peer educators attached to health facilitiesWaelimishaji rika kwenye vituo vya afya
  • Tracing and welcoming back members who stopped treatmentKuwafuatilia na kuwakaribisha waliokatisha matibabu
  • Community feedback on the quality of careMaoni ya jamii kuhusu ubora wa huduma

Stigma & discriminationUnyanyapaa na ubaguzi

Stigma keeps people away from testing, from treatment and from disclosure. We measure it, name it and work with communities, employers and the media to reduce it.

Unyanyapaa huwafanya watu waepuke kupima, kutibiwa na kuwaeleza wengine hali zao. Tunaupima, tunauweka wazi na tunafanya kazi na jamii, waajiri na vyombo vya habari kuupunguza.

  • The PLHIV Stigma Index in TanzaniaKipimo cha Unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU
  • Community dialogues with leaders and familiesMajadiliano ya jamii na viongozi na familia
  • Training journalists on reporting about HIVKuwapa mafunzo waandishi wa habari kuhusu VVU

Economic empowermentUwezeshaji kiuchumi

Medicine works better on a full stomach. Savings and lending groups, skills training and small business support help members build an income that survives illness.

Dawa hufanya kazi vizuri tumbo likiwa na chakula. Vikundi vya akiba na mikopo, mafunzo ya ujuzi na msaada wa biashara ndogo huwasaidia wanachama kujenga kipato kinachostahimili ugonjwa.

  • Village savings and lending groupsVikundi vya akiba na mikopo vijijini
  • Vocational and entrepreneurship trainingMafunzo ya ufundi na ujasiriamali
  • Linking groups to markets and financeKuunganisha vikundi na masoko na taasisi za fedha

Adolescents & young peopleVijana balehe na vijana

Young people living with HIV face disclosure, school, dating and treatment fatigue all at once. Youth-led groups give them somewhere to take those questions.

Vijana wanaoishi na VVU hukabiliana kwa wakati mmoja na kuwaeleza wengine, shule, mahusiano na uchovu wa dawa. Vikundi vinavyoongozwa na vijana huwapa mahali pa kupeleka maswali hayo.

  • Youth peer groups and mentorshipVikundi vya vijana na ushauri wa wenzao
  • Support through transition to adult careMsaada wakati wa kuhamia huduma za watu wazima
  • Sexual and reproductive health informationElimu ya afya ya uzazi na ngono

Community systems strengtheningKuimarisha mifumo ya jamii

A network is only as strong as its weakest district. We train and equip regional and district networks so they can plan, report and hold services to account on their own.

Mtandao ni imara kadri ya wilaya yake dhaifu zaidi. Tunaimarisha mitandao ya mikoa na wilaya ili iweze kupanga, kutoa taarifa na kuwajibisha watoa huduma yenyewe.

  • Governance and financial management trainingMafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha
  • Community-led monitoring of HIV servicesUfuatiliaji wa huduma za VVU unaoongozwa na jamii
  • A single membership register for the whole countryDaftari moja la uanachama kwa nchi nzima

How we workJinsi tunavyofanya kazi

Members firstWanachama kwanza

Every programme is designed with the people it serves, not for them.

Kila programu hubuniwa pamoja na wale inaowahudumia, si kwa niaba yao.

Evidence, not anecdoteUshahidi, si masimulizi

We collect data from our own networks so our advocacy stands up to scrutiny.

Tunakusanya takwimu kutoka mitandao yetu ili utetezi wetu usimame kwenye uchunguzi.

Confidentiality alwaysUsiri wakati wote

Health information stays private. No member's status is ever shared without consent.

Taarifa za afya hubaki siri. Hali ya mwanachama haisambazwi bila ridhaa yake.

Work with usFanya kazi nasi

Funders, government partners and civil society organisations - we would like to hear from you. Wafadhili, wadau wa serikali na asasi za kiraia - tungependa kusikia kutoka kwenu.

Get in touchWasiliana nasi