Dar es salaam, Tanzania
Leo tarehe 4 Februari 2024, katika viwanja vya Mbagala Zakhiem, yalifanyika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Saratani Duniani yakiongozwa na Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume.
Washiriki na Wadau
Maadhimisho haya yaliratibiwa na kushirikisha wadau mbalimbali wa afya wakiwemo:
- NACOPHA
- Taasisi ya Saratani Ocean Road
- TAMISEMI
- WHO
- TAS
- Mashujaa Cancer Foundation
Yote haya yalifanyika chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya kwa kauli mbiu isemayo, “Saratani Inazuilika Huduma Sawa kwa Wote.”
Shughuli za Kiafya
Katika maadhimisho haya, kulikuwa na shughuli mbalimbali za kiafya zikiwemo:
- Upimaji na uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi, tezi dume, na saratani ya matiti
- Utoaji wa damu salama
- Upimaji wa shinikizo la damu na kisukari
- Huduma nyingine nyingi za kiafya
Uzinduzi wa Afya Game
Aidha, kulikuwa na uzinduzi wa Afya Game, mchezo wa bahati unaolenga kuchangia huduma za afya kwa wagonjwa wa saratani huku ukitoa nafasi za kushindia zawadi mbalimbali. Wageni mbalimbali walichangia huduma hii kwa moyo mkunjufu.
Hotuba ya Mgeni Rasmi
Mgeni rasmi, Dkt. Rashid Mfaume, alitambua kazi kubwa inayofanywa na NACOPHA katika mwitikio wa UKIMWI na mchango mkubwa wa WAVIU katika ufuasi mzuri wa dawa. Pia, alitambua ushiriki wa NACOPHA katika uzinduzi wa mpango jumishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Kwa habari zaidi na updates, tafadhali tembelea tovuti yetu au fuatilia mitandao yetu ya kijamii.